Soga
Sera ya Faragha
Taarifa gani tunakusanya, kwa nini, na tunazishiriki na nani.
Sera hii inaeleza jinsi NETPOA LTD inavyokusanya na kutumia taarifa zako binafsi unapotumia Soga (soga.tz). Tunakusanya taarifa chache tu tunazohitaji ili kukupa huduma.
1. Taarifa tunazokusanya
| Taarifa | Kwa nini |
|---|---|
| Namba ya simu | Kukuingiza kwa namba ya siri (OTP), kukutumia risiti, na (kwa waandishi) kukulipa |
| Jina | Kukutambua kwenye akaunti na risiti |
| Barua pepe na picha ya Google (ukiingia na Google) | Kukuingiza na kuonyesha picha yako |
| Picha ya wasifu (ukipakia) | Kuonyesha kwenye akaunti yako na, kwa waandishi, kwenye ukurasa wa umma |
| Historia ya malipo: kiasi, kumbukumbu, njia ya malipo, risiti ya mtandao | Kuthibitisha malipo, kutoa huduma, kutatua matatizo, na kutimiza sheria za kodi |
| Historia ya usomaji: sura ulizosoma, hadithi ulizopenda, waandishi unaowafuatilia | "Endelea kusoma", Maktaba yako, na kugawa mapato ya vifurushi kwa waandishi kwa haki |
| Taarifa za kiufundi: anwani ya IP, aina ya kivinjari, vidakuzi (cookies) vya kikao | Usalama, kuzuia matumizi mabaya, na kukuweka umeingia |
| Kwa waandishi: jina la kalamu, maelezo, jina lililosajiliwa kwenye M-Pesa | Kuonyesha kazi zako na kukulipa |
Hatukusanyi wala kuhifadhi PIN za mobile money au namba za kadi. Hizo zinashughulikiwa na mtoa huduma wa malipo.
2. Tunavyotumia taarifa
- Kukupa huduma uliyoomba (kuingia, kusoma, kulipa, kulipwa).
- Kukutumia ujumbe muhimu: namba za siri, risiti, taarifa za maombi ya kutoa pesa.
- Usalama: kuzuia udanganyifu na matumizi mabaya.
- Kuboresha huduma kwa takwimu za jumla (mfano hadithi zinazosomwa zaidi).
Hatuuzi taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote, na hatutumii namba yako kwa matangazo bila idhini yako.
3. Tunaowashirikisha taarifa
Tunashiriki taarifa na watoa huduma wanaotusaidia, kwa kiasi kinachohitajika tu:
- Cheko (Netpoa Limited): kushughulikia malipo na malipo kwa waandishi.
- POASMS (Netpoa Limited): kutuma SMS na ujumbe wa WhatsApp. Ujumbe wa WhatsApp hupita kwenye mfumo wa Meta (WhatsApp).
- Google: ukichagua kuingia na Google.
- Mtoa huduma wa seva (hosting): taarifa zinahifadhiwa kwenye seva zinazoweza kuwa nje ya Tanzania. Tunachukua hatua za kuzilinda (tazama Ulinzi wa Data).
- Mamlaka za kisheria: pale tunapolazimika kisheria.
4. Kwa waandishi: taarifa za umma
Jina la kalamu, picha, maelezo, hadithi, idadi ya wafuatiliaji na alama ya uthibitisho vinaonekana kwa umma. Namba ya simu na jina la malipo havionekani kwa umma.
5. Vidakuzi (cookies)
Tunatumia vidakuzi muhimu tu: kukuweka umeingia, kulinda fomu (CSRF), na kukumbuka chaguo lako la hali ya giza. Hatutumii vidakuzi vya matangazo.
6. Muda wa kuhifadhi
- Taarifa za akaunti: kwa muda wote akaunti ipo.
- Kumbukumbu za malipo: kwa muda unaotakiwa na sheria za kodi na uhasibu, hata baada ya akaunti kufutwa.
- Namba za siri (OTP): zinafutwa ndani ya siku 7.
- Kumbukumbu za kiufundi (logs): hadi siku 14.
7. Haki zako
Una haki ya kuona, kusahihisha au kufuta taarifa zako, na zaidi. Maelezo kamili yako kwenye ukurasa wa Ulinzi wa Data.
8. Watoto
Huduma inalengwa kwa watu wa miaka 18 au zaidi. Watoto wanapaswa kuitumia kwa idhini na usimamizi wa mzazi au mlezi.
9. Mawasiliano
Maswali kuhusu faragha: info@netpoa.com NETPOA LTD, P.O.BOX 62228 DAR ES SALAAM
Imesasishwa: 16/11/2026