✍️ Kwa waandishi wa Kiswahili
Andika. Chapisha.
Lipwa.
Geuza hadithi zako kuwa kipato. Wasomaji wanalipa kusoma, nawe unapata 60% ya kila mauzo, moja kwa moja kwenye simu yako.
Hakuna ada ya kujiunga · Unabaki na hakimiliki ya kazi yako
Mapato mwezi huu
TZS 384,000
5.2K
Views
320
Mauzo
890
Followers
Mfano wa dashboard ya mwandishi
60%
ya kila mauzo ya hadithi yako
+ Mgao
wa vifurushi kila mwezi
TZS 11,500
kiwango cha chini cha kutoa
Siku 1–3
pesa kufika kwenye simu yako
Jinsi unavyopata pesa
Njia mbili za kipato
1. Mauzo ya hadithi zako
Unaweka bei ya hadithi nzima. Kila msomaji anapoinunua, 60% ni yako. Ada ya malipo inalipwa na msomaji, haikatwi kwako.
Mfano: bei TZS 2,000
2. Mgao wa vifurushi
Wasomaji wenye kifurushi wanasoma hadithi zote. Kila mwezi, 60% ya mapato yote ya vifurushi yanagawanywa kwa waandishi kulingana na sura za kulipia zilizosomwa kwenye hadithi zao.
Maana yake:
Hadithi zinazosomwa zaidi zinapata mgao mkubwa zaidi, hata kama msomaji hakuinunua moja kwa moja.
Kokotoa kipato chako
Sogeza vitelezi uone unavyoweza kupata kwa mauzo ya hadithi peke yake.
Unaweza kupata kwa mwezi
TZS 180,000
Kwa mwaka
TZS 2,160,000
Hii ni makadirio tu; mapato halisi yanategemea wasomaji. Mgao wa vifurushi ni ziada juu ya hiki.
Rahisi kuanza
Kutoka wazo hadi pesa, hatua 4
-
1
Jiunge
Ingia kwa namba yako ya simu, jaza jina la kalamu. Dakika 2 tu.
-
2
Andika
Jina, muhtasari, utangulizi, kisha "Weka sura ya kwanza", "ya pili"… hatua kwa hatua.
-
3
Chapisha
Weka bei na sura za bure. Timu yetu inakagua na kukujulisha kwa WhatsApp au SMS.
-
4
Lipwa
Fuatilia mauzo kwenye dashboard, toa pesa kwa M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas na HaloPesa.
Kila kitu unachohitaji kukua
Ukurasa wako binafsi
soga.tz/a/jina-lako: hadithi zako zote mahali pamoja, rahisi kushiriki.
Wafuasi (Followers)
Wasomaji wanakufuata na wanaona hadithi zako mpya kwanza.
Takwimu za kila siku
Views, mauzo na mapato kwa kila hadithi, kwenye dashboard yako.
Zana za uandishi
Panga aya kwa kubofya mara moja, leta hadithi nzima, na msaada wa AI.
Alama ya bluu ✓
Waandishi waliothibitishwa wanapata alama ya kuaminika.
Kazi yako inalindwa
Unabaki na hakimiliki. Maandishi hayanakiliwi kirahisi na sura za kulipia zimefungwa.
Maswali ya mara kwa mara
Je, kujiunga kunalipiwa?
Hapana. Kujiunga na kuchapisha ni bure. Tunapata sehemu yetu tu pale hadithi zako zinapouzwa.
Hakimiliki ya hadithi yangu ni ya nani?
Ni yako. Kwa kuchapisha unatupa ruhusa ya kuonyesha na kuuza hadithi hiyo kwenye Soga tu.
Nitalipwa vipi na lini?
Mapato ya mauzo yanapatikana baada ya siku 7 za usalama. Ukifikia TZS 11,500, bofya "Toa pesa" na tunatuma kwa M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas na HaloPesa ndani ya siku 1–3 za kazi.
Bei ya hadithi naiweka mimi?
Ndiyo. Unaamua bei na idadi ya sura za bure. Unaweza pia kuweka hadithi bure kabisa ili kujenga wafuasi.
Je, lazima nimalize hadithi yote kabla ya kuchapisha?
Hapana. Chapisha sura chache kwanza, kisha ongeza nyingine. Wasomaji wataona hadithi "Inaendelea".
Hadithi yangu inakaguliwa kwa nini?
Kuhakikisha ubora na kwamba maudhui yanafuata masharti. Ikihitaji marekebisho tunakutumia maoni.
Naweza kuandika kwa simu?
Ndiyo. Kila kitu kimetengenezwa kufanya kazi vizuri kwenye simu.
Maelezo kamili: Taarifa kwa waandishi
Hadithi yako inastahili wasomaji.
Jiunge leo, chapisha sura ya kwanza, na uanze kujenga wafuasi na kipato chako.
Jiunge kama mwandishi, ni bure